TANZANIA

Je wafahamu!...Jumla ya  eneo  lenye  ukubwa wa kilomita za mraba  242,000 ambapo  ni sawa  na asilimia  28 ni eneo  lililotengwa  maalumu  kwa ajili  ya uhifadhi  wa maliasili  pamoja  na maumbile  yake  asilia  ya Kijiografia  katika nchi  yenye  ukubwa wa eneo  lenye  kilomita  za mraba  945,641. Maeneo  haya  ya uhifadhi  wa maliasili  pamoja na maumbile  yake asilia  ya  kijiografia  yamegawanyishwa  katika maeneo  tofauti tofauti  ukitofautiana  kutokana na kiwango  chake  kimuhimu, kiuhitaji, ulinzi na uhifadhi  katika maeneo  husika  pamoja na  wanyamapori wake  na maumbile ya asili.
Maeneo  haya ya uhifadhi wa mali  asili  pamoja na maumbile  yake  asilia ya kijiografia   ni kama vile;

Hifadhi za Taifa  (National parks) 
Hifadhi za bahari  zenye fukwe 
Eneno pekee nchiniTanzania la hifadhi  mseto  ya  mamlaka ya hifadhi  ya Ngorongoro  (Ngorongoro  conservation Area Authority).
Urithi wa Dunia  (world  heritagesites).
Maeneo  ya rasilimali ya Akiba (resource  reserves) kama vile  mapori  ya akiba  ya wanyamapori,  misitu  ya asili  pamoja na  vitalu  vya  uwindaji  wa wanyamapori.
Maeneo ya  bainowai  yanayotambuliwa  na  kusimamiwa   na shirika  la  umoja  wa mataifa  linaloshughulikia Elimu, sayansi na  utamaduni (UNESCO) pamoja na maeneo  mengineyo  tofauti  tofauti. 
Ikumbukwe  na  ieleweke  kwa umma wa  watanzania wote  nchini  ya kwamba  baadhi  ya maeneo  haya   ya uhifadhi  wa maliasili   nchini  Tanzania   yamebuniwa  na kupewa  hadhi  na shirika  la umoja  wa mataifa  linaloshughulikia Elimu , sayansi na utamaduni   (UNESCO)  kama urithi  wa  dunia  pamoja na maneno  ya  bainowai  ikimaanisha  ya kwamba  si yenye  umuhimu   wakipekee  tu  kwa nchi  yetu  Tanzania  lakini  vile vile  ni muhimu  kwa faida  ya Dunia  nzima

Mifano ya maeneo  ya  uhifadhi  wa maliasili  nchini Tanznaia ambayo  ni  urithi  wa Dunia  (world  heritage sites) ni  kama vile; 
Mamlaka  ya hifadhi ya Ngorongoro
(ngorongoro conservation Area Authority – NCAA) ikihusisha  maeneno  yake  zaidi  kama vile  bonde la Ngorngoro  (ngorongoro  crater.)
Empakai  crater (bonde la Empakai) pamoja  na Bonde la Olduvai  (Olduvai Gorge)
maarufu  ikijulikana  kama “Oldupai”. 
Magofu  ya majengo  ya kale  ya  kihistoria  yanayopatikana  kilwa  kisiwani  na Songo mnara.
Hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti 
Pori la  akiba  la wanyamapori  la Selous  ( selous  Game Reserve). 
Hifadhi  ya Taifa  ya mlima  Kilimanjaro
Mji Mkongwe  Zanzibari  (the stone  town  of Zanzibar. 
Hifadhi za bahari  zenye  fukwe 
Kisiwa  cha  mafia  katika bahari  ya hindi  chenye  upekee wa aina yake
Fukwe za manzi na Ruvuma  pamoja na fukwe za  Mkwaja  Saadam.

Mifano ya maneno ya uhifadhi wa mali asili  nchini Tanzania  yanayotambuliwa  kama maeneo ya bainowai na Shirika la umoja  wa mataifa  linalishughulikiwa Elimu , sayansi  na Utamaduni  (United  Nations  Educational,  scientific  and cultureal  organizations).

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU