TAARIFA KWA UMMA WA WATANZANIA WATALII WA NDANI

DONDOO

Kama moja  ya sehemu ya matukio yenye   kuwa na umuhimu  mkubwa  katika  historia  ya  nchi  yetu  Tanzania katika  kuadhimisha  miaka 50  ya uhuru wa Taifa  letu Tanzania Desemba   9,2011, Seriakali  yetu ya  Jamhuri   ya Muungano  wa Tanzania  iliwaalika na  kuwakaribisha  mabalozi  wote wa  ndani ya  Tanzania  wanaofanya  kazi  na  kuziwakilisha nchi zao  katika  ardhi ya Tanzania  katika kutembelea  vivutio vyetu asilia  ya  utalii Tanzania  na hii  ilikuwa  ni pamoja  na hifadhi maarufu duniani ya Serengeti ipatikanayo  katika  Mkoa   wa Mara.

Safari  hiyo ya  mabalozi  wa nchi za nje wnaofanya  kazi  ndani ya Tanzania  ilichukua  takribani  mabalozi  32,  wakuu wa mikoa  nchini  Tanzania pamoja na maofisa wanaowakilisha Makampuni makubwa  yaliyowekeza nchini Tanzania katika  kutembelea  hifadhi ya  Taifa  ya Serengeti, Bonde la Ngorongoro (Ngorongoro creater) katika  mamlaka ya hifadhi  ngorongoro na sehemu  ya  unyayo wa binadamu wa  kale  wa  Lactoti vile vile  katika  mamlaka  ya hifadhi ya Ngorongoro.

Sehemu nyinginezo  katika  matembezi  ya   mabalozi  ya  mabalozi  hao ilikuwa  ni pamoja  na  fukwe  za  visiwa  vya Zanzibar  vipatikanavyo katika bahari  ya hindi  na vile  vile  safari ya matembezi yao iliwapeleka katika  Kijiji cha Butiama  kipatikanacho  katika  mwambao  wa Ziwa  Victoria  katika Mkoa  wa  Mara, Sehemu  ambayo  ndipo alipozaliwa  Muasisi wa Taifa  letu la  Tanzania,  Hayati  Baba wa Taifa   Mwalimu Julius  Kambarage  Nyerere   takribani  miaka  89 iliyopita.

Waziri wa mambo  ya nchi za nje na  ushirikiano wa  kimataifa  mheshimiwa  ndugu  Bernard Membe  ndiye  aliyekuwa  kiongozi  Mkuu wa msafara  huo wa  matembezi katika   kuwaongoza  mabalozi   wa nchi  za nje   wanaofanya  kazi  nchini  Tanzania  katika  kuziwakilisha  nchi zao katika  kutembelea  vivutio asilia  vya  utalii   vipatikanavyo katika kanda ya  Kaskazini kama vile  hifadhi  ya ziwa  Manyara  pamoja na hifadhi  ya mlima Kilimanjaro katika  Mkoa wa Kilimanjaro. Mheshimiwa   ndugu Bernard  Membe alisema  ya  kwamba  malengo makubwa  ya safari  hiyo  maalumu  ya mabalozi  ilikuwa  ni  kuitangaza  Tanzania  kwa mabalozi  wa nchi za nje  wanaofanya  kazi  Tanzania  ili waweze  kuwa  mabalozi  wazuri wa kuitangaza  nchi yetu Tanzania kwa mataifa  yao  ili  wananchi  wao  waeze  kutembelea  nchi yetu Tanzania.

 


SISI CHUO CHA  UTALII  CHA UDZUNGWA  TUNAMPONGEZA  MHESHIMIWA  NDUGU  BERNARD MEMBE  KWA HATUA ALIZOZICHUKUA  KWA  VITENDO  KATIKA   KUTANGAZA   NCHI YETU NA  KWA SABABU HII NDIO  ILIYOPELEKEA  SISI KUTIZAMA  UPANDE  WA PILI WA  SHILINGI  KATIKA  KUITANGAZA TANZANIA KWA  WATANZANIA  WATALII  WA NDANI  NA  KUWEZA  KUANZISHA TAMASHA LETU LA UELIMISHAJI, UHAMASISHAJI NA  UWEZESHAJI  UTALII WA NDANI  NCHINI  TANZANIA  LITAKALOJULIKANA  KAMA  “TAZAMA  RAMANI  TANZANIA  FESTIVAL” .

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU