wasifu wa mikoa

WASIFU WA MKOA WA MANYARA
                                                       "Maskani ya Madini ya Tanzanite"

UTANGALIZI
Mkoa  wa Manyara  ulianzishwa  baada ya kutenganishwa  kutoka  katika  Mkoa wa   zamani  wa Arusha  katika  mwaka 2002.

Ikumbukwe  na ieleweke ya  kwamba  kuanzishwa  kwa Mkoa  mpya  wa Manyara  ulitangazwa  rasmi  katika  gazeti  la Serikali  namba  367 mwezi Julai  2002. Makao Makuu ya Mkoa  wa Manyara   ni  Mji  wa  Babati ambao  unapatikana  takribani   kilomita  167 kutoka  katika  jiji la Arusha  na  ambapo  ni sawa  na  umbali wa  takribani  kilomita  157 kutoka  Mkoani  Singida na vile  vile  ni umbali wa  takribani  kilomita   248 kama  unatokea  Mkoani  Dodoma.   

KIUTAWALA
Mkoa  wa Manyara  umegwanyishwa  katika   Wilaya   5  ambazo  ni  Wilaya  ya  Babati, Hanang,  Kiteto, Mbulu pamoja na  Wilaya  ya Simanjiro kwa  ujumla  Mkoa wa Manyara  una  tarafa  29, Kata  123 na  vijiji 293.

HALMASHAURI YA WILAYA YA SIMANJIRO
Halmashauri  ya Wilaya  ya Simanjiro ni  moja  kati ya Wilaya  5  zinazounda  mkoa wa Manyara  na  inapakana kimipaka   na Wilaya  za Moshi, Hai na Arumeru katika upande wa  Kaskazini, Wilaya  ya  kiteto katika upande wa  Kaskazini, Wilaya  ya Kiteto katika  upande wa Kusini, Wilaya za  kondoa  na Babati katika  upande wa Magahribi  wakati ambapo  Wilaya  za  Mwanga, Same,  Kilindi pamoja na  Korogwe ni  katika  upande wa Mashariki. Halmashauri  ya Wilaya  ya Simanjiro  ilianzishwa rasmi  mnamo  mwaka  1993 kwa  mujibu wa sheria  yta Bunge  la Jamhuri  ya Muungano  wa  Tanzania.

 Ukubwa wa eneo lake  Wilaya  ya Simanjiro
Halmashauri ya Wilaya  ya Simanjiro  ina ukubwa  wa eneo  lenye  kuwa na  kiomita  za mraba  takribani  20,591. 

Jiografia  yake  na Hali ya Hewa
Halmashauri  ya Wilaya ya Simanjiro Kijiografia   inangukia  katika  maeneo  makame   ya uoto  wa asili  iliyotawaliwa  na miti ya   migunga  na maeneo   wazi  yaliyotawaliwa   na uoto wa  nyasi  (Somali – Maasai region). Wastani  wa  mvua  katika mwaka  mzima  kama  jinsi  ilivyo  katika maeneo  mengineyo katika  ukanda  huu  ni  milimita  300 mpaka  700.  Kuna  misimu   miwili  ya mvua   ambapo  ni  mvua za  vuli  (mwezi  Novemba hadi  Desemba).  Na  mvua za masika  ni  katika  kipindi  kati ya  mwezi  Machi  hadi  mwezi  Aprili. 

Kipindi  cha baridi  ni kati ya  mwezi  Mei  hadi  mwezi  Julai  na kipindi  cha  nyakati  za joto ni kati  ya mwezi  Agosti  hadi  Februari . kiwango  cha joto  ni kati  ya  nyuzi  joto  13  mpaka  30.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU