Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli  kuhusu Hifadhi  ya Ziwa  Manyara:
Jina  la hifadhi ya Taifa  ya ziwa Manyara  limetokana na neno lililotoholewa  kutoka  katika lugha ya kabila la Wamaasai (Emanyara) lenye  kumaanisha  mmea wa asili  ujulikanao  Kiswahili kama ‘Mnyaa. Kisayansi na Kibotania mmea  huu  unafahamika  kama (Eurphorbia tirucalii) na  katika lugha  ya  Kiingereza unafahamika kama  (Milk bush  au  Finger  Eurphorbia) na  huwa  unatoa  utomvu  mweupe  ambao  ukipenya  katika  macho  huleta  upofu. Mimea  mingineyo ambayo  ni jamii  au kundi la EURPHORBIA ni pamoja  na mmea unaofahamika  MTOMVU (Eurphorbia Candelabram) katika  lugha ya Kiingereza.

Jamii ya Kabila la Wamaasai  hutumia mmea huu  katika kutengeneza uzio wa  maboma  yao wanayoyatumia  kama makazi. Hifadhi  hii inapatikana  katika mji  maarufu  wa Kitalii  wa mto wa mbu  katika  Mkoa wa Arusha  na hifadhi hii ya taifa ya ziwa  Manyara  inapatikana  ndani  ya Bonde la  ufa la Mashariki.

manyara

MAANDALIZI YA USAFIRI
Maandalizi ya  usafiri yazingatie  huduma za malazi au  kulala,  chakula, usafiri wenyewe  na mengineyo mengi  yaliyo muhimu.

KUANZISHWA KWAKE;
Hifadhi ya Taifa ya ziwa Manyara ilianzishwa  mwaka 1960. Hifadhi hii  iliyoanzishwa  mwaka mmoja  kabla  ya uhuru wa nchi yetu  ina hadhi ya Kimataifa kutokana na umuhimu wake wa kipekee  kwa faida  ya dunia  nzima kama eneo  la  bainuai inayotambuliwa  na Shirika  la umoja  wa mataifa  linaloshughulikia  Elimu, Sayansi na utamaduni (UNESCO). Mwandishi  maarufu wa Kimarekani wa  nyakati  hizo  aliyejulikana  kama Ernest Hemingway alivutiwa sana na mandhari  yenye  muonekano  wenye  kupendeza  katika  hifadhi  na ambayo  ndiyo  iliyompelekea yeye  mwenyewe  kuandika  katika  Kitabu  chake  kilichojulikana  kama  “Green hills of Africa”.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU