Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli  kuhusu TARANGIRE:
Hifadhi ya Taifa ya Tarangire  ilipata  jina lake  hilo  kutokana na mto Tarangire ambao  chanzo  na asili yake  kimeanzia  maeneo  ya nyanda  za juu  za mto Kondoa  upatikanao  katika Mkoa wa Dodoma. Urefu wa mto  Tarangire  ni Kilomita  120  na mto  huu umepitia  katikati  ya hifadhi  hii. Hifadhi ya Taifa  ya Tarangire Kijiografia  inapatikana  katika  Mkoa wa Arusha, Mji  ambao  ndio  kitovu  cha Utalii nchini  Tanzania.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Watanzania  wazalendo watalii wa ndani  ni  lazima watambue  ya kwamba  fedha  zinahitajika  katika  maandalizi  ya usafiri  na upatikanaji  wake  unahitaji  mipango  mkakati. Waanze  na bajeti  ya mahitaji  ya fedha  na makadirio  ya gharama za safari  ya matembezi  hifadhini.
Bajeti  ya mahitaji  ya fedha  izingatie  kwa umakini  mkubwa wa mtiririko  wa mambo  yafuatayo kama vile  huduma  za  malazi  au  kulala,  chakula, usafiri na mahitaji mengineyo muhimu  yanayoweza  kujitokeza kama vile  dharura.

KUANZISHWA  KWAKE:
Ilianzishwa mnamo  mwaka 1970. Kabla  ya kuanzishwa  kwake  kama hifadhi  ya Taifa  ilikuwa  ni moja  ya eneo  la  pori  la akiba la wanyamapori  na lililo kuwa  maarufu kwa shughuli za uwindaji  wa Wanyamapori  kwa kibali  maalumu  kinachoruhusu uwindaji.

ENEO LAKE:
Ukubwa wa eneo la hifadhi  hii ni  kilomita za mraba  2850.

UFIKAJI  HIFADHINI:
Hifadhi  ya Taifa ya Tarangire inafikika  kwa njia ya usafiri  wa barabara  umbali  wa kilomita  120  Kusini  Magharibi  mwa  Mji wa Arusha  katika barabara  kuu ya  Arusha – Dodoma.  Vile vile  ni sawa na  umbali  wa Kilomita  95  Kusini  Mashariki mwa  hifadhi  ya ziwa Manyara. 
Inapatikana pia umbali wa Kilomita  155 kutoka mamlaka ya hifadhi  ya Ngorongoro na vile vile  ni umbali  wa kilomita  300 kutoka  hifadhi  ya Taifa  ya Serengeti. Ni sawa  na umbali wa saa moja  kutoka  Arusha  Mjini  na saa 3  mpaka  4  kutoka  hifadhi  ya Taifa ya Serengeti. 

MAUMBILE ASILIA  YA KIJIOGRAFIA HIFADHINI:
Mto Tarangire, kanda  za uoto  wa asili, maeneo yenye  ardhi oevu, vilima na  Majabali ya  mawe  pamoja  na miti  mingi ya mibuyu iliyotawanyika sehemu  mbalimbali  hifadhini.

HALI YA HEWA  USAWA WA BAHARI  HIFADHINI.
Inaanzia  mita 1,100 mpaka 1500 kutoka  usawa wa Bahari.

VIVUTIO  VIKUU VYA UTALII HIFADHINI:
Eneo la migunga mwanvuli (Acacia tortilis parkland), chatu wapandao juu ya miti, makundi mengi ya tembo  au (ndovu), mto Tarangire, maeneo yenye  Ardhi  Oevu, miti ya mibuyu, aina  kadhaa mbalimbali  za viumbe  hai  ndege  na  sura ya mandhari ya eneo.

WANYAMAPORI WAPATIKANAO  HIFADHINI
Ni pamoja na Wanyamapori kama vile  Tembo (Ndovu),  Pundamilia,  Nyati  (mbogo), Swala pala, Twiga,  Nyani, Ngedere (Tumbili), Swala tomi, Swala granti, Kuro,  Mbweha Masikio, Simba, Chui, Choroa, Kongoni aina ya Cokei,  nyumbu, pofu, Tohe, digidigi (Saruya) na wengineo  wengi.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU