Hifadhi ya Saadani

Ukweli  kuhusu hifadhi  ya Taifa  ya Saadani:
Hifadhi ya Taifa  pekee  nchini  Tanzania  na  Afrika  ya Mashariki yenye  fukwe za bahari  na inayotazamana na Bahari  ya Hindi.  Ni  hifadhi pekee  ambapo  fukwe za bahari  zake  zinakutana  na uoto wa asili  wa nchi kavu. 

          Uwepo wa hifadhi  ya Taifa  ya Saadani  ni  matokeo  ya pori  la akiba  la Saadani,  ranchi ya  mkwaja  na sehemu ya Kaskazini ya mkwaja  sambamba na  akiba  ya msitu wa asili wa Zaraninge. Hifadhi  hii inapatikana baina ya  Mkoa wa Tanga na Pwani.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Ni pamoja  na kufahamu  gharama za jumla  za  safari  yenu  ya  matembezi  hifadhini  Saadani.

          Ufahamu  wa maandalizi  haya  yazingatie  mambo  muhimu  ya Kimsingi  kama vile  Usafiri, Sehemu za huduma za chakula, malazi au kulala na  mengineyo yatakayojitokeza .
Baada ya  haya  yote  kutekelezwa  kwa  ukamilifu na umakini  mkubwa  kitakachofuatilia  ni mpango  mkakati  wa fedha  za maandalizi  zilizopatikana. Mwisho  kabisa  ni  bajeti  ya fedha  za maandalizi  kuandaliwa  jinsi  zilivyopangiliwa.

KUANZISHWA KWAKE:
Ilianzishwa  mwaka 2005. Tangu  miaka  ya 1960,  eneo hili  la Saadani  ilikuwa  ni moja  ya maeneo  ya pori la  akiba la wanyamapori.

ENEO LAKE:
Ukubwa wa eneo la hifadhi  ya Taifa  ya Saadani  ni  ukubwa  wa eneo  la kilomita  za mraba  1,178. Nchi  kavu  inachukua  ukubwa  wa kilomita  za mraba  1,148 na  kilomita  za mraba  30  ni eneo  la maji  ya bahari  ya hindi. 

UFIKAJI HIFADHINI;
Hifadhi  ya Taifa ya Saadani  inafikika  umbali  wa kilomita  50  kutoka  visiwa vya Zanzibari  na inachukua saa 3  kwa  njia ya usafiri wa majini wa kutumia  ngalawa  na  vile vile  ni  dakika  takribani  50 kwa njia  ya usafiri wa majini  wa  kutumia  boti. Vile vile  ni sawa  na kilomita   45  kutoka  mji  wa kihistoria  wa Bagamoyo.( dakika 40) na Dar es salaam ni  kilomita 100.

MAUMBILE  ASILIA  YA KIJIOGRAFIA HIFADHINI: 
Tambarare  za pwani,  vilima vidogo vidogo, mlima  kiono unaohifadhi  msitu wa asili wa zaraninge  kwa upande  wa kusini  Magharibi.

          Upande wa Kaskazini wa Mkwaja  una mandhari nzuri  yenye  kupendeza  ya makazi  ya vilima  vya hapa na pale. Kwa  upande wa kusini  ni Bonde  la mto  Wami.

HALI YA  HEWA  USAWA WA BAHARI  HIFADHINI:
Inaanzia  0 mpaka  350  kutoka  usawa wa bahari. 

VIVUTIO  VIKUU VYA  UTALII HIFADHINI:
Fukwe  na Bahari, kasa  wenye  viota  vya  mayai  ardhini katika eneo la  madete. Vile vile  mto  wami  una  aina  mbalimbali  za wanyamapori na ndege,  mikoko pamoja na maji  ya bahari  yanayokutana  na mto  (Estuaries). 

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
walio tembelea

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU