Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli kuhusu hifadhi ya Taifa ya Visiwa vya  Rubondo:
Hifadhi ya Taifa  ya Visiwa  vya Rubondo  ni hifadhi  pekee nchini Tanzania na barani Afrika  ipatikanayo katika makazi ya  maji ya ziwa  Victoria.  Kijiografia  hifadhi hii  inapatikana  katika ziwa  Victoria,  Kaskazini mwa Ghuba  ya  Emini Pasha Mkoani  Mwanza.  Hifadhi  hii ya  Taifa  ya visiwa vya Rubondo ilianzishwa  mwaka  1977. Ni  hifadhi  ambayo  imezungukwa  na visiwa  kadhaa  kama  vile   Mizo, Nyamitundu,  Chitende, Rubiso,  Chitebe, Kalera,  Iroba, Chambuzi, Manyila,  Makosi pamoja na izilambuba.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Ni pamoja na upatikanaji  wa fedha  zitakazotumika kuwezesha   na kufanikisha  safari  za matembezi  hifadhini   na bajeti  yake  ilivyopangiliwa.

KUANZISHWA KWAKE:
Ilianzishwa mwaka 1977.

ENEO LAKE:
Ukubwa wa eneo la hifadhi ya visiwa vya Rubondo ni kilomita za mraba   457. Kilomita  za  mraba  237 ni nchi  kavu na kilomita  za mraba  220  ni  maji.

UFIKAJI  HIFADHDINI:
Hifadhi  hii inafikika kwa njia ya   usafiri  wa maji  ya ziwa  Victoria  takribani  kilomita  165  baada ya njia  ya barabara  kupitia  Sengerema,  Geita na  nzera.  Ni  umbali wa  saa 6  mpaka 7.

MAUMBILE  ASILIA  YA KIJIOGRAFIA  HIFADHINI:
Ziwa  Victoria,  visiwa  takribani  11 vinavyozunguka  hifadhi  yenyewe; majabali  mawili  makubwa  ndani ya  Ziwa, moja  upande wa  Kaskazini  na  jingine   upande wa Kusini  pamoja na msitu.

HALI YA HEWA USAWA WA BAHARI HIFADHINI:
Inaanzia mita 1, 134 kutoka usawa wa Bahari 

VIVUTIO VIKUU VYA UTALII HIFADHINI:
Ziwa  Victoria,   viumbe  hai  ndege  wahamao,  Fukwe, idadi  kubwa  ya mwewe walao samaki (fish  eagles),  Nzohe pamoja na idadi  kubwa ya viumbe  hai  vipepeo.

WANYAMAPORI WAPATIKANAO HIFADHINI:
Mamba, Nguchiro wa makazi ya ardhi oevu,  panya walao  miwa,  saruya au digidigi, ngiri, kuro, Tumbili, kindi, Twiga, viboko,  Tembo, nguruwe mwitu, sokwe mtu,  nyati au  mbogo pamoja na wanyamapori  wengineo jamii ya  nyani (PRIMATES).

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU