Hifadhi ya Taifa ya Katavi

Ukweli Kuhusu Hifadhi ya Taifa ya Mikumi:
Hifadhi ya Taifa ya mikumi inapatikana katika Mkoa wa Morogoro.  Ni  moja  kati ya hifadhi za Taifa  nchini Tanzania  zinazopatikana   upande wa Kusini  (Southern  circuits).  Ni umbali   wa takribani  kilomita  295 magharibi mwa  Mji wa Dar – es  - Salaam  kufika katika  hifadhi  hii.  Hifadhi  hii ya  Taifa  ya Mikumi  ni hifadhi  ya nne (4)  kwa ukubwa  wa eneo  nchini Tanzania.  Vile vile  hifadhi  hii  inapatikana  baina ya miji ya Doma na Mikumi  katika  barabara  kuu ya Dar es  Salaam Tunduma.  Makao makuu ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi inapatikana kutoka usawa wa bahari  mita  549. Ilianzishwa  mwaka  1964 na ilipata  jina lake  hilo  kutoka  katika  Mji wa  Mikumi   ambapo kiasili halisi  cha jina  hili  kinatokana na  mimea  ya miti ya jamii ya minazi  ijulikanayo Kiswahili  kama mchapa. 

          Katika Mabila mengineyo nchini Tanzania kama vile Wasukuma na Wanyamwezi mmea huu wa mti unajulikana kama Muhama.

MAANDALIZI YA USAFIRI
Kabla ya  maamuzi  kuchukuliwa  kutembelea  hifadhini  ni  vema  maandalizi ya  usafiri  ya  matembezi  hifadhini  yakapewa  kipaumbele  cha kwanza  ikizingatiwa  ya kwamba  gharama za usafiri hupanda  mara  kwa  mara  nchini  Tanzania. 

KUANZISHWA KWAKE:
Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ilianzishwa mnamo mwaka 1964.

ENEO LAKE: 
Ukubwa wa eneo  la  hifadhi  ya Taifa ya  Mikumi  ni kilomita  za mraba  3,230.

UFIKAJI  HIFADHINI:
Hifadhi  ya Taifa  ya Mikumi  inafikika  kwa njia ya usafiri  wa barabara  umbali wa takribani  kilomita  295 kutoka  Dar es salaam na vile vile  ni sawa  na umbali  wa  kilomita  330  kutoka  hifadhi  ya Taifa  ya  Ruaha.  Ni saa 3 mpaka 4 kutoka Dar –es – salaam na ni saa 5 mpaka 6 kutoka Ruaha.

MAUMBILE ASILIA YA KIJIOGRAFIA HIFADHINI: 
Tambarare  za mto Mkata, maeneo  yenye  ardhi  oevu  na vile vile  uoto  wa asili  wa miti  ya Miombo. 

HALI YA HEWA USAWA WA BAHARI HIFADHINI:
Inaanzia mita 500 mpaka 1257 kutoka usawa wa Bahari.

VIVUTIO VIKUU VYA UTALII HIFADHINI:
Tambarare  za mto  mkata,  Wanyamapori Tembo,  Twiga,  mbwa mwitu na wengineo mbalimbali,  viumbe  hai ndege  wahamao  na maeneo ya  Kitamaduni.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
free hit counter

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU