Hifadhi ya Taifa ya Gombe

Ukweli kuhusu Hifadhi ya Gombe:
Hifadhi ya Taifa  ya GOMBE ni hifadhi iliyoanzishwa  maalumu kwa ajili  ya  tafiti  za Kisayansi  hususani  katika kuwalinda  na kuwahifadhi Wanyamapori adimu  wa jamii  ya Sokwe mtu  (chimpanzees) ambao wapo  hatarini   kutoweka  duniani (Endangered species). 

          Hifadhi  hii ya Gombe  ilianzishwa  rasmi mwaka 1968 mkoani  Kigoma  katika  mwambao  wa ziwa Tanganyika, upande  wa mashariki  takribani  umbali wa kilomita  24  kwa njia ya usafiri wa maji ya Ziwa Tanganyika Kaskazini mwa Mji wa  Kigoma. 

 Hifadhi   hii imegawanyishwa katika kanda  4  ambazo  ni pamoja  na kanda za fukwe , kanda za ziwa,  kanda za maeneo  ya mapori, msitu  na utawala wa hifadhi.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Hiki ni kipaumbele  nambari  moja  kuliko  vyote  ambacho  hutoa  muelekeo na taswira  ya uwepo  wa  safari ya  matembezi  hifadhini au hapana.  Aina  ya  usafiri  utakaotumika  kufika hifadhini  na gharama zake. Haya yote  yanahitaji  fedha. 

KUANZISHWA KWAKE:
Hifadhi ya Taifa ya Gombe ilianzishwa mnamo mwaka 1968.  Kijiografia  hifadhi hii  ya Gombe  inapatikana  Mkoani  Kigoma,  upande wa magharibi mwa nchi  yetu  Tanzania. 

ENEO LAKE: 
Ukubwa wa eneo la hifadhi ya Taifa ya Gombe ni kilomita za mraba 52. Kuna  uwezekano  wa mpango  hapo baadaye  wa  kuliongeza  eneo  la hifadhi  hii.

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
walio tembelea

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU