Hifadhi ya Taifa ya Arusha

Ukweli  kuhusu  hifadhi  ya Taifa  ya Arusha:
Hifadhi  ya Taifa ya Arusha  na Mkoa  wa Arusha  umepata  majina  yake  kutoka katika  Kabila la Waarusha  ambayo  ni  mojawapo  ya Makabila  ya jamii  ya Wabantu. Waarusha  na Makabila  mengineyo  ya Mkoa wa Arusha  kama  vile  Wameru  na Wamaasai, yamekuwepo  yakiishi  maeneo ya hifadhi   hii  Kihistoria  kwa miaka mingi  sana ya Mababu na Mabibi. Kihistoria  moja ya Makabila  mengineyo ambayo  yamepata  kuishi  katika  hifadhi  hii  ni  pamoja na  kabila la Wachaga.

Hifadhi  hii ilianzishwa  mwaka 1960,  mwaka  mmoja  kabla ya Uhuru wa nchi  yetu na ni  hifadhi pekee Tanzania  ambayo imepata  kubadilisha  majina  yake  takribani  mara tatu.  Mwanzoni  kabisa  ilikuwa  ikiitwa hifadhi  ya Taifa  ya bonde la Ngurdoto (Ngurdoto  crater National  Park) kutokana na bonde la Ngurdoto kama moja ya maeneo  ya  maumbile  ya  kijiografia  hifadhini yenye kuwa na  vivutio vya kupendeza.  Baadaye  tena jina  la Ngurdoto likabadilishwa  na kuitwa  hifadhi  ya Taifa  ya Mlima  Meru (Meru  crater National  Park) na  hatimaye  mwaka  1967 jina la hifadhi ya Taifa  ya Arusha  likatumika rasmi  mpaka  hadi leo. Hifadhi hii inapatikana Mkoani Arusha.

MAANDALIZI YA USAFIRI:
Mambo ya kuzingatiwa  na kupewa  kipaumbele  cha hali  ya juu  kabisa  ni  maandalizi ya  usafiri  kama vile gharama  za Usafiri hifadhini  kwenda na kundi  iwe usafiri  binafsi au wa kukodi,  huduma za  malazi au  kulala,  chakula pamoja  na mahitaji  mengineyo yatakayojitokeza. Haya yote  yanahitaji fedha na namna  ambayo  hizo  fedha  jinsi  zitakavyotumika. Fedha hizo  zinahitaji  kutengenezewa  bajeti  ya matembezi  hifadhini.

maandalizi ya safari

soma zaidi

Watch-Tanzanian-Map ____________________________________________________________________________________________________

BLOGU NA HABARI ZA UTALII
TAARIFA KWA UMMA
KUTOKA KWA MKURUGENZI MTENDAJI
MAKABILA YALIYOPO TANZANIA
WASIFU WA MIKOA KIUTALII
MATUKIO NA MATAMASHA
HAMASIKA
MAONI
JARIDA
UOTO WA ASILI
WATOTO
WITO WETU
USAFIRI
RAMANI
MAKTABA YA PICHA
Fortune Media Work
Simu: +255654002397
www.fortunemediawork.com | © 2011-2014
Tazama Ramani Tanzanian. Haki zote zimehifadhiwa
walio tembelea

logos NgorongoroS!TE TATOTz EAC UDMCT TTB TANAPA KARIBU